URA walivyoanza kutetea Ubingwa wao vs KVZ Jan 1 2017

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi timu ya URA ya Uganda jumapili ya January 1 2017 ilishuka uwanjani kucheza dhidi ya KVZ katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi A, hiyo ikiwa ni sehemu ya harakati zao za kuanza kutetea taji lao.
dsc_0009
URA wameendelea kupata matokeo chanya kama mwaka 2016 katika uwanja wa Amaan kwa kufanikiwa kuifunga KVZ goli 2-o, magoli ambayo yalifungwa na Lapama Bogota dakika ya 57 na 90.

URA wanapata nafasi ya kuongoza Kundi A kwa tofauti ya goli moja dhidi ya Taifa Jang’ombe wakati huu ambapo yanasubiriwa matokeo ya mchezo wa Simba dhidi ya Taifa Jang’ombe.
Mpya zaidi Nzee zaidi