Handeni. Kamati za maji katika mitaaya Kata ya Mlimani, Halmashauri ya Mji wa Handeni, zimetakiwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi yatokanayo na mradi huo.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kuunda kamati mpya ya maji ya Mtaa wa Kwasindi jana, Diwani wa kata hiyo, Mwajabu Suphiani alisema tatizo la kamati nyingi kujisahau kuwa zimewekwa na wananchi.
Alisema imekuwa desturi kila kamati inayoundwa kukumbwa na tatizo la kushindwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya mradi, huku wengine wakipingana na viongozi wao kuhusu uwazi wa matumizi ya fedha hizo ambazo ni za wananchi.
Hivi karibuni, Mbunge wa Handeni Mjini, Omari Kigoda alisema kama kamati hizo zimeshindwa kusoma mapato na matumizi zivunjwe na ziundwe nyingine.