MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA UKIMWI YAMEFIKA NJIA PANDA

MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA UKIMWI YAMEFIKA NJIA PANDA
Mpaka hivi sasa imepita miaka ………tangu nchi yetu ilipoanzisha rasmi vita dhidi ya ukimwi na hivyo kuanzishwa kwa taasisi maalum inayoendelea navita hiyo Kupitia mikakati na program mbalimbali hii inamaana ya kwamba serikali yetu kupitia wizara ya afya na taasisi ya mapambano dhidi ya ukimwi imekuwa ikitekeleza mipango mbalimbali ikiwemo uhamasishaji wa jamii, utoaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (ARVS) na kadhalika
Hata hivyo mipango yote hiyo inayotekelezwa imekuwa ikifadhiliwa na nchi hisani kutoka ulaya na mamarekani kwa 97%

Shukrani nyingi kwa ushirikiano huu uliodumu kwa muda wa miaka Zaidi ya 15 watu wengi waliotambuliwa kuwa waathirika wa ukimwi wameweza kupata huduma za dawa ya ARVS na hivyo kuweza kapata nafasi ya kuongeza maisha yao kadri ilivyowezekana

Kama ubora wa takwimu zinazotolewa na mamlaka husika ni ule unaofaa kuchukuliwa kama msingi wa mjadala wetu basi inaarifiwa ya kwamba watu wapatao 1.4 milioni nchini wanaishi na virusi vya ukimwi kati ya watu hao waathirika ni asilimia 50%ndio wenye kupata tembe za ARV au watu wapatao laki nane kwa upande mwingine inafahamishwa ya kwamba kasi ya maambukizi ya vizusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa motto imepungua kwa asilimia 50%

MAFANIKIO DHAIFU
Kwa vyovyote vile mafanikio haya yaliyo yaliyopatikana siyo ya kubeza hata kidogo ukilinganisha nachangamoto iliyokuwepo wakati mapambano dhidi ya ukimwi yalipoanzishwa

JUKUMU KUBWA LINALO KABILI MAMLAKA HUSIKA NA WADAU WENGINE NI KUHAKIKISHA MAFANIKIO HAYO YANATUNZWA BILA KURUDI
Hata hivyo itakuwa ni kazi  changamoto ya ziada kadri muda unavyopita kuyatunza mafanikio hayo na hata kupiga hatua nyingine kuelekea kwenye matuamini ya ushindi wa vita hii ukizingatia mtazamo  wa mamlaka na wadau wakati wote huu

Hii ni kwa sababu wakati wa mabadiliko ya kisera na kisiasa yanafanyika kila uchao katika nchi hisani,wanatunga sera na mikakati ya maendeleo ya kijamii nchini mmwetu wanabaki wale wateja wa mipango iliyobuniw aya zamani

TATIZO HILI LINAHATARI YA KUZOROTESHA PAKUBWA KASI KASI TULIYONAYO KUSITISHA MISAADA/UFADHILI YA VITA DHIDI YA UKIMWI
Habari za kuaminika zinabainisha kuna uwezekano mkubwa yakatokea mabadiliko katika nchi hisani yatakayopelekea kusitishwa kwa ufadhi wa mifuko mbalimbali inayogharamia vita dhidi ya ukimwi na hivyo kuwacha pengo kubwa ambalo itakuwa si rahisi kwa rasilimali za ndani kulijaza na kuendelea kutekeleza mipango iliyokuwepo na hata mipya kama mabadiliko mhayo yatatokea basi ni wazi yanauwezekano mkubwa wa kuziacha mamlaka zetu za afya na taasisi za mapambano dhidi ya ukimwi katika hali ya huzuni na inayodhihirisha ya kwamba kuna udhaifu mkubwa kati majopo ya wataalamu wetu pale wanapotakiwa kufanya kazi ya kubuni mipango  madhubuti na endelevu kwa ajili ya kuboresha afay aya mwanadamu

Hususani mipango hiyo inayobuniwa iwe yenye uwezo wa kubainisha mikakati ya kuendeleza na kujenga rasilimali za ndani na hivyo kpata njia ya kujitegemea mara tu wafadhili watakapositishwa

TIBA ASILI NI RASILIMALI MUHIMU YA NDANI
Kwa maoni yetu na uzoefu wa matukio mbalimbali ya maendeleo ya tiba asili duniani. tr msigwa anaamini kama tukiweza katika mali asili yetu ya ndani tutakuwa tumepata jawabu katika matatizo hayo yanayoikabili jamii

Iwe ni kwa sababu ya uvivu au kutojiamini ,au kutotambua matokeo ya kujikita katika mipango tegemezi ya mapambano dhidi ya ukimwi hayaleti dalili nzuri kamwe na huenda yakazoroteshwa pakubwa kasi ya maendeleo yaliyopatikana mpaka sasa izingatiwe yakwamba endapo tangu mwanzo wa mapambano ya ukimwi ingalikuweko nia ya ukweli miongoni ya taasisi husika kuendeleza tiba asilia kwa kubuni mikakati ya ukweli na makusudi inyolenga kuleta matokeo ya tija kuelekea upatikanaji wa dawa ya ukimwi au kinga yake basi ingewezekana mafanikio hayo kufikiwa
Kinyume chake katika nchi yetu mchango wa tiba asiilia unatambuliwa kinadharia pekee unaposoma vitabu vya sera,magazeti au kuhudhuria semina mbalimbali

Wakati mkapambano yakipamba moto chini ya ufadhili mnono kutoka nchi hisani tumeshuhudia maelekezo ya aina mbalmbali kutokea taasisi za tiba na utafiti wa dawa za mwanadamu yakikataza kutangaza madai yoyote ya tabibu wa tiba asili kuhusu uwezo wa dawa anayotengeneza kutibu ugonjwa wa ukimwi achilia mbali uwezo wa kuleta nafuu

Matangazo kama hayo kutoka kwa tabibu wa tba asili yanachukuliwa kama kitendo cha uhaini dhidi ya mapambano ya ukimwi yanayoendelea kwa maneno mengine masharti kama haya yanaweza punguza uwezo wa kupata tiba ya ukimwi kutokana na tiba asilia ambazo ni rasilimali yetu yanaleta mtazamo uliodhahiri ya kwamba:iwe iwavyo bora tukubali shida na changamoto zinazoongezeka katika utoaji huduma za maradhi ya ukimwi huku tukisubiria wahisani watakavyoamua kuliko kufikiri kwamba siku moja dawa ya ukimwi itapatikana nchini Tanzania kwa ajili ya matumizi ya watu wake

BAADA YA MPANGO TEGEMEZI TUSHIKE MTI GANI
Baada ya harakati za kutekeleza mpango wa vita dhidi ya ukimwi uliotegemezi na bila kitengo cha kujenga misingi imara ya rasilimali za ndani sasa hatuna budi kusimama na kutafakari mti gani wa kushika au njia gani ya kupita ili tuweze kufika kwenye lengo letu la kushinda maradhi ya ukimwi nchini Tanzania

HIVI SASA MUDA SI RAFIKI
Kwa kuwa tumetumia mda mrefu kutekaleza mpango wa vita dhidi ya ukimwi bila tahadhari ya kujenga na kutimiza misingi imara ya rasilimali za ndani haitakuwa jambo rahisi kukubaliana na changamoto za mapambano hayo katika muda unatakiwa na kupata matokeo yenye tija kwa wakati

KUCHANGIA MFUKO MAALUM WA VITA DHIDI YA UKIMWI
Kwa haraka katika mazingira haya ni rahisi kubuni wazo la kuchangia mfuko maalum wa vita dhidi ya  ukimwi nchini Tanzania.kama njia ya kulinda mafanikio yetu wazo hili limedhihirika na kuamuliwa hivi karibuni tarehe ……………wakati ulipobuniwa mfuko maalum wa fedha kwa mapambano dhidi ya ukimwi mpaka sasa waendeshajio wa mfuko huu wanatenga michango ya hiari kutokea sekta binafsi kama njia moja ya kutumisha mfuko huu, kama ilivyo mifuko mingine kama hiyo inahitaji muda wa  kujijenga na kutimiza malengo yake mbalimbali, Si rahisi kutamka ni lini mfuko huu utakuwa umejijenga vya kutosha ili kukidhi mahitaji yaliyopo katika maeneo mbalimbali ya vita dhidi ya ukimwi.wakati tukisubiri maendeleo ya mfuko huu changamoto zilizo katika mapambano dhidi ya ukimwi zinaendelea kuimalika. Takwimu zinazotolewa na tasisi ya mapambono dhidi ya ukimwi linasema ya kwamba kunaongezeko la asilimia 5% ya kusambaa kwa maambukizi mapya ya ukimwi kila mwaka hii ni sawa na maambkizi ya watu wapatao 100,000 kila mwaka

JE UJIO WA CHANJO DHIDI YA UKIMWI NI SULUHISHO!
Katika mazingira magumu tunayo kabiriana nayo ni rahisi kufikiri ya kwamba ujio wa chanjodhidi ya ukimwi utakuwa suluhisho la kudumu laa hasha, ni vema ieleweke ya kwamba mchakato wa kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya ukimwi unakaribiana na changamoto za kipekee ambazo azipatikani katika majaribio ya chanjo nyengine hii ni kwa sababu ya kwamba chanjo ya ukimwi inajaribiwa katika mwili wa binaadamu anaye kuwa na hatari ya kuporomoka kwa kinga haraka kinyme na chanjo nyingine  ya majaribio ya maradhi kama vile POLIO, SURUA, na kadhalika, kama vile haitoshi ieleweke ya kwamba hata kama chanjo hiyo dhidi ya ukimwi itafanikiwa haina maana ya kwamba maradhi hayo yatatokomwzwa moja kwa moja.laa hasha ieleweke ya kwamba virusi huweza kurudi na kuishi hii imeshuhudiwa katika mazoezi ya usambazaji wa chanjo mbalimbali kama vile SURUA, POLIO N.K. Maeneo mengine yaliyo tambuliwa na shiko la umoja wa mataifa kama hayana hatari ya maradhi surua na polio hivi sasa yamepata mlipuko mkubwa. Hivyo ukizingatia mambo yote haya niwazi ya kwamba bado nchi yetu inakibarua kikubwa katika vita dhidi ya ukimwi. Moja ya mafunzo tuliyopata katika kipindi kilichopita ni kwamba ipo haja ya kuendeleza rasilimali zetu wenyewe ndani za FEDHA, UFUNDI, UTAALAMU, ili kupata safu kamili ya askari wa kupambana na maradhi ya ukimwi.

BACTERIA WA CHINI YA BAHARI KUWA DAWA MAGONJWA SUGU
Hivi karibuni wataalamu wa maradhi ya kibinadamu nchini uingeleza wametangaza kupatikana kwa tiba inayoweza kusaidia wagojwa wa maradhi kama ya HEWA au MISHIPA Y FAHAMU ILIYOATHILIKA pamoja na SARATAN kutokana na dawa inayotengenezwa kwa kutumia bacteria anayepatika chini ya bahari mafanikio kama haya yanaonyesha ni jinsi gani mtalamu wa kweli anavyoweza kupambana bila kukata tamaa ili kuhakikisha ya kwamba matatizo ya maradhi ya naweza kutatuliwa  kwa kutumia viumbe hai vinavyoonekana na visivyo onekana kwa macho ya kawaida. Mafanikio kama haya ni ushahidi tosha ya kwamba tiba asilia ambazo kimsingi na mimea, mitishamba, vyakula, wanyama na  ndege n.k. ni moja ya m aeneo yanayoweza kuleta nafuu ya tiba kwa wagojwa kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe za ndani , ileweke ya kwamba kwa muda mrefu uliopita tiba asilia imekuwa ikitumia maji ya bahari kuwa kama dawa kwa maradhi mbalimbali.

Kwa ushauri na maoni kuhusu dawa na mambo mengine mpigie
0713646691
0752819047
0773149272
0787677215
Mungu ibariki afrika mungu inariki tanzania mungu mbariki tr msigwa.

ANGALIA VIDEO HII..

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia