Tanzia: kamanda wa polisi wa zamani mkoa wa kilimanjaro dkt. Mohamed chico afariki dunia

Kamanda wa polisi wa zamani mkoa wa kilimanjaro Dkt. Mohamed  Chico amefariki Dunia  usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salam.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia Bw. Awadhi Chico, mazishi yake yamepangwa kufanyika leo Jumapili 22/01/2017 jioni katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Kijitonyama. Habari ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo.

Mwenyezi Mungu amjaalie kauli thabit na ailaze roho yake mahali pema peponi - AMIN
INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJI'UN
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia