Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadick amepiga marufuku utengenezaji wa pombe za kienyeji kwa kutumia nafaka kama mahindi na mtama.
Akiongea na waandishi wa habri Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadick amewataka wananchi kuhifadhi mazao yao na kuhakikisha wanauza chakula kilicho cha ziada tu na si vinginevyo.
Pia Said Mecky Sadick amedai kuwa kwa sasa wameanza kuweka msisitizo katika kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula kutumia kilimo cha umwagiliaji.
"Mkoa umepiga marufuku matumizi ya kutengeneza pombe ya kienyeji kwa kutumia nafaka ikiwemo mahindi pamoja na mtama, vile vile wananchi tunawahimiza kutumia chakula walichokivuna vizuri, waendelee kuuza ziada na wananchi wenye mifugo tunawashauri kuvuna baadhi ya mifugo yao mfano kuku, mbuzi, ng'ombe kuuza na kupata fedha na kujinunulia chakula sasa hivi wakati bei bado ikiwa chini" Said Mecky Sadick