Usiku wa Jumanne hii Instagram ilikumbwa na mafuriko ya live, saa chache baada ya huduma hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kuzinduliwa kwa watu wote.
Wengine walikesha wakiwa live, na wengine wameamka nayo asubuhi. Tangu ilipotangazwa November mwaka jana, huduma hiyo ilikuwa inapatikana katika sehemu chache tu duniani.
Baada ya Instagram live kukamilika, video hiyo haiwezi tena kupatikana na watumiaji, tofauti na huduma zingine ambapo video inaweza kuhifadhiwa na kutazamwa baadaye.
Instagram live videos zinaweza kutumia zaidi ya saa nzima.
