Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), jana lilitangaza tuzo hiyo inayotolewa kila mwezi kwenda kwa nyota huyo raia wa Zimbwabwe baada ya kuwashinda kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima na beki wa Azam raia wa Ivory Coast, Yakubu Mohamed waliokuwa wakiwania pia tuzo hiyo.
Kwa Desemba mechi tatu zilichezwa huku vinara Simba wakicheza mechi mbili kati ya hizo ugenini na moja ikicheza nyumbani.
Mwanjale aliiongoza Simba kushinda mechi zote tatu, hivyo timu yake kupata ushindi wa asilimia 100 kwa kunyakua pointi zote tisa, na kubaki katika nafasi yao ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Aidha, katika mwezi huo Simba haikufungwa bao hata moja huku Mwanjale akicheza dakika zote 90 katika mechi zote sawa na jumla ya dakika 270, pia hakuonyeshwa kadi yoyote kwenye michezo hiyo.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Mwanjale atazawadiwa fedha, kiasi cha Shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo, Kampuni ya Vodacom Tanzania.
Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mchezaji bora kwa msimu wa 2016/2017 hadi sasa ni John Raphael Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Ramadhan Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba), na Rifati Hamisi wa Ndanda (Novemba).
JIUNGE NASI KATIKA
YOUTUBE @Muungwana Tube
BOFYA HAPA KU-INSTALLAPP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.