
Nyota wa kimataifa wa mchezo wa tenisi Serena Williams achumbiwa .
Serena mwenye umri wa miaka 35 ameripotiwa kuchumbiwa na Alexis Ohanian mwenye miaka 33.
Taarifa zaidi zafahamisha kuwa Serena alichumbiwa Alhamis katika hafla maalum iliyoandaliwa na mchumba wake jijini Roma Italia .
Katika hafla hiyo mchumba wake alikariri shairi kabla ya kumvisha pete ya uchumba .