Serikali kuwanyang'anya mashamba wakulima Muheza ilikuweka utaratibu bora wa ardhi.

Serikali wilayani Muheza imeandaa mchakato wa kuwanyang'anya mashamba wakulima zaidi ya 1000 waliopo katika vijiji vinne vilivyopo kata za Mtindiro na Kwafungo ili kuweka utaratibu wa matumizi bora ya ardhi kisha kuyamega na kuwapatia wakazi ambao hawana kabisa maeneo ya ardhi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Buhuri kilichopo kata ya Mtindiro wilayani Muheza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji, mkuu wa wilaya ya Muheza Eng'mwanasha Tumbo amesema mashamba hayo ambayo yalifutiwa hati na Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni lengo lake ni kuwamegea wananchi ili kuondokana na migogoro ya ardhi inayoweza kuzuilika.

Akielezea hali ya ukame inayowakabili wakazi wa eneo hilo, diwani wa kata ya Mtindiro Mustapher Ayoub amesema msimu wa kilimo umekaribia hivyo wameiomba serikali kuharakisha kuwapelekea mbegu kwa sababu wakazi zaidi ya 1000 wa kata hiyo hawana hata mbegu baada ya kuzitumia kwa sababu ya uhaba wa chakula unaowakabili wakazi wa eneo hilo.

Kufuatia hatua hiyo, mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na usalama ndani na nje ya nchi Mheshimiwa Adad Rajab amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia vyema mradi wa maji uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 33 ambao umefadhiliwa na msamaria wema kwa lengo la kuwapunguzia changamoto wakazi wa kata hiyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items