Uchimbaji mchanga kwenye makazi ya watu Wizara yataka wananchi kutoa taarifa NEMC

Baadhi ya Wakazi wa Tegeta sala sala waishio eneo la Kilimahewa jijini Dar es salaam, wamelalamikia kitendo cha uchimbaji mchanga unaofanywa katika eneo lao hivyo kutishia uharibifu wa mazingira.

Kwa masharti ya kutopigwa picha na kurikodiwa sauti zao, wananchi hao wameelezea masikitiko yao ya uchimbaji mchanga kwenye eneo la makazi ya watu na hivyo kutishia uharibifu wa mazingira yanayozunguka eneo la Kilimahewa, huku wakieleza kuwa juhudi za kuwasiliana na mamlaka ngazi ya eneo hilo zimeshindwa kukomesha tatizo hilo.

Channel ten imeshuhudia baadhi ya magari yakiingia kuchukua mchanga, na ilipofuatilia ngazi ya wizara, waziri mwenye dhamana ya mazingira amewataka wananchi hao kuchukua hatua haraka za kulipeleka suala hilo kwenye baraza la taifa la Usimamizi za Mazingira-NEMC.
Mpya zaidi Nzee zaidi