Ushahidi Dhidi ya Mkurugenzi wa ATCL Waendelea Kisutu

Aliyekuwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka, akishuka ngazi za Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake iliyoahirishwa.

 USHAHIDI dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi  Mtendaji  wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka,  umeendelea leo  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  baada ya kamera yetu kumnasa akitoka kujibu kesi yake ya tuhuma  za kughushi  na  matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara

Kesi hiyo imeahirishwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Respicius Mwijage,  hadi Machi 3 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa serikali dhidi yake.
Mpya zaidi Nzee zaidi