Video: JPM Aendesha Basi la Abiria la Mwendokasi kwenye uzinduzi

Rais Dk. John Pombe Magufuli amezindua rasmi miundombinu ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam – DART ambapo amewataka mawaziri na watendaji wa mradi huo wanaohusika na suala la mapato kumpatia mchanganuo wa mapato yaliyopatikana tangu kuanza kwa utoaji wa huduma ya mpito ya usafiri kuanzia mwezi May mwaka jana.

Rais Magufuli amesema wananchi wanataka kujua kama mradi huo unaendeshwa kwa faida au hasara kwa kuwa kiasi cha fedha shilingi bilioni 403 zilizotumika katika utekelezwaji wa mradi ambazo kati ya hizo bilioni 317 ni mkopo kutoka benki ya dunia na bilioni 86 zimetolewa na serikali hivyo amezitaka mamlaka husika kupeleka mchanganuo huo ifikapo leo jioni.

Amesema endapo angepata mchanganuo huo angeziagiza mamlaka husika kujenga kituo kingine eneo la kimara kwa ajili ya maegesho ya magari madogo kwa ajili ya kutoa fursa ya watumiaji wa mabasi hayo kuacha magari yao na kuingia kwenye mabasi kuelekea maeneo mbalimbali lakini pia kujenga kituo cha daladala katika eneo hilo hilo kwa ajili ya kuwapunguzia adha abiria wanaotoka nje ya mji.

Aidha amewataka waendesha mradi hukakikisha abiria hawakai muda mrefu vituoni wakisubili usafiri huku akiiomba banki ya dunia kuharakisha utoaji wa msaada wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya mandela na morogoro ubungo ili kuondoa uchelewashaji wa mabasi hayo katika eneo jambo ambalo linaondoa dhana nzima ya mabasi yaendayo haraka.

Katika taarifa yake mtendaji mkuu wa DART mhandisi Leonard Lwakatare amesema fedha zilichopatikana kuanzia may 10 huduma ya mpito ilipoanza hadi mwezi desemba mwaka jana kuwa shilingi bilioni 3.39.

Naye waziri wa nchi TAMISEMI George Simbachawene amesema mradi huo ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo masuala ya umiliki wa hisa, ambapo hata hivyo mmiliki wa asilimia 51 ya hisa za UDA kampuni ya Simon Group ilikubali kulipa kiasi cha shilingi bilioni 5.8 kwa ajili ya hisa hizo fedha ambazo mpaka sasa ziko kwenye mvutano wa matumizi yake. Rais Magufuli ametoa siku 5 kuhakikisha wahusika wanapanga matumizi yanayolenga maendeleo na wakishindwa atapanga mwenyewe.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha