VIDEO: Walichokisema CCM kuhusu madai ya baa la njaa nchini

Wakati mengi yakizungumzwa kuhusiana na madai ya kuwepo kwa baa la njaa nchini na baadhi ya maeneo kuripotiwa kuwa vyakula vimepanda bei kutokana na ukame uliosababishawa na kukosekana kwa mvua.

Leo January 2017 Chama cha Mapinduzi kupitia kwa katibu wake wa itikadi na uenezi wa Humprey Polepole amezungumza na waandishi wa habari kuhusu suala hilo.

‘Baa la njaa si kitu kidogo, ni jambo kubwa kabisa inapofika nchi imekumbwa nalo, mwenye dhamana ya mwisho kutangaza ni mkuu wa nchi na anapotangaza anatumia dhamana yake kama mkuu wa nchi kwamba tunayo njaa lakini hapa Tanzania Mungu ametubariki katika zaidi ya miaka 25 iliyopita hatujafika kiwango hicho‘


Mpya zaidi Nzee zaidi