Wafugaji Babati waigomea serikali

Screen Shot 2017-01-22 at 3.09.04 PMWafugaji kabila la Wabarbeig katika kijiji cha Vilima Vitatu wilayani Babati ambao wamekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu baina yao na serikali ya kijiji, wamegoma kuondoka kwenye katika eneo wanaloishi ambalo ni sehemu ya hifadhi ya jamii ya ziwa Burunge hata baada ya serikali kupitia upya mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Wananchi hawa wameyatoa hayo mbele ya kamati ya Mifugo,Kilimo,na Maji ya bunge ambayo imetembelea katika kijiji hiki cha vilima vitatu kutaka kujua juu ya mgogoro huo baina ya serikali yakijiji na wafugaji hawa.

Ajabu na mshangao ikajitokeza katika mkutano wa kamati ya bunge na wananchi wa vilima vitatu mara baada ya moja ya wawekezaji waliopo katika eneo hili kuomba kuondolewa kwa madai kuwa wao ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya kijiji hiki.

Wajumbe wa kamati ya mifugo,kilimo na maji ya bunge ikatoa ushauri kuumaliza mgogoro huu.

Na hii ndiyo taarifa ya mkoa wa manyara juu ya mgogoro wa vilima vitatu.
Mpya zaidi Nzee zaidi