Waliokuwa watumishi BoT wapigwa danadana za kisheria

Dar es Salaam. Watu 31 waliokuwa wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) bado wanaendelea kukumbwa na danadana za kisheria baada ya benki hiyo kupeleka tena ombi Mahakama Kuu ili kesi hiyo ipitiwe upya.

Oktoba 2, mwaka jana Mahakama Kuu iliwapa ushindi wafanyakazi hao waliosimamishwa kazi mwaka 1993 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni programu ya kuimarisha uchumi.

Wakili wa wafanyakazi hao,  Barnabas Luguwa alisema alipokea barua juzi kutoka BoT ikuhusu ombi la kutaka kesi ipitiwe upya.

“Nimepokea barua yao kwa kifupi bado wanaomba muda uongezwe katika kesi hii na wanataka ipitiwe upya,” alisema Wakili Luguwa.

Alifafanua kuwa ni zaidi ya mara nne kwa BoT kuomba waongezewe muda kesi ipitiwe upya tangu ilipoanza kusikilizwa miaka 22 iliyopita.

Hata hivyo, BoT walipeleka barua Mahakama Kuu Novemba mwaka jana wakiomba hukumu hiyo ipitiwe upya, ombi hilo lilitupiliwa mbali.

Lakini juzi, BoT walipeleka tena ombi kuomba kesi hiyo ipewe muda na kupitiwa upya.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items