Wanafunzi wa chuo cha uuguzi na ukunga zaidi ya 200 wameingia katika siku ya pili ya mgomo wa kutoa huduma za vitendo katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo pamoja na nadharia kufuatia mabweni yao kukatwa maji na umeme kwa kipindi kirefu hatua ambayo wamedai kuwa imesababisha wataalam hao wa afya kuathirika magonjwa yatokanayo na uchafu.
Ni wanafunzi wa chuo cha uuguzi na ukunga jijini Tanga ambao wamelalamikia kusitishwa kwa huduma hizo kwa takribani miezi kumi hadi sasa hatua ambayo imesababisha kuweka mgomo ikiwa ni sehemu ya kuishinikiza serikali kurudishiwa huduma hizo ili kuwanusuru na magonjwa yanayoweza kuzuilika pamoja na usalama wa maisha yao hasa nyakati za usiku.
Hata hivyo mkuu wa chuo hicho Thomas Marato na makamu wake Jacob Mwakasekele wakielezea hatua hiyo wamesema hadi jioni hii walikuwa katika mchakato wa kulipia huduma ya umeme pamoja na maji ili huduma kwa wanafunzi hao ziweze kuendelea.