Watanzania waalikwa kuwekeza Mji wa Ras Al Khaimah watajwa kuwa na fursa za utalii

KINYUME na ilivyozoeleka kuwa mataifa yaliyoendelea ndiyo yanayopaswa kuja kuwekeza nchini, hali imekua tofauti baada ya Serikali ya Falme za Kiarabu (UAE) kupitia mji wa Ras Al Khaimah kuwaomba Watanzania kwenda kuwekeza katika mji huo wa kitalii.

Akizungumza katika hafla ya utambulisho wa fursa za kibiashara kwenye mji huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa mipango uhusiano na ushirikiano wa maendeleo ya kibiashara katika kituo cha RAK International Corporate, Shankar Bharathan amesema wafanyabishara kutoka ukanda huu wanakaribishwa kwenda kunufaika na uwekezaji usio na mipaka

Kwa upande wake mmoja wa wahudhuriaji wa hafla hiyo ya utambulisho Elinisaidie Msuri kutoka kampuni ya MEKONSULT, amewaomba watanzania kutumia fursa hiyo kuwekeza katika eneo la ghuba.

RAK International Corporate Centre ni mamlaka iliyo katika mji wa Ras Al Khaimah iliyoanzishwa kutokana na muunganiko wa kampuni mbili za RAK International Companies ambayo awali iliitwa RAK Free Trade Zone na RAK Offshore ambayo awali ilikuwa sehemu ya RAK Investment Authority.

JIUNGE NASI 
 INSTA@MUUNGWANABLOG ,FB@MUUNGWANABLOG,YOUTUBE @MUUNGWANA TUBE, BOFYA HAPA KU-INSTALL APP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.
Mpya zaidi Nzee zaidi