Kikosi cha Mzambia George Lwandamina, Yanga kinatarajiwa kushuka dimbani kesho kukipiga na Ashanti United kwenye mchezo wa kombe la FA unaotakaofanyika katika uwanja Uhuru.

Yanga wanashuka dimbani wakiwa ni mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kumfunga Azam 3-1 kwenye fainali ya kwanza tangu michuano hiyo iliporejeshwa tena.
Akizungumza na shaffihdauda.co.tz kocha msaidizi Juma Mwambusi amesema: “Tumejianda vizuri nia yetu ni kushinda na tuna matumaini na vijana wetu watajituma kulinga na tuliyowafundisha ili kutetea kombe letu.”
“Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri huku wakiwa na morali ya kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri katika michuano hiyo ambayo ipo katika hatua ya tano.”
Aidha Timu hiyo itawakosa baadhi ya nyota wake ambao ni Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Justin Zullu, Malimi Busungu ambaye bado ana matatizo ya kifamilia.
JIUNGE NASI
INSTA@MUUNGWANABLOG ,FB@MUUNGWANABLOG,YOUTUBE @MUUNGWANA TUBE, BOFYA HAPA KU-INSTALL APP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.