ACT yaandaa kongamano la azimio la Arusha

Dar es Salaam.  Chama cha ACT Wazalendo kimeandaa mjadala wa Kitaifa utakaohusisha wanasiasa wa vyama mbalimbali vya  ndani na nje ya nchi, wanazuoni na wanaharakati  kujadili misingi na miiko ya Azimio la Arusha iliyofutwa mwaka  1992 na Halmashauri Kuu ya CCM.

Chama hicho kimesema lengo la kuandaa mkutano huo ni kutokana na  Utawala uliopo madarakani na uliomaliza muda wake kuendesha nchi bila kufuata misingi ya kisheria na kanuni za uongozi ambazo zilikuwa ndani ya azimio la Arushwa kabla ya kufutwa.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo, Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alisema, “Matatizo ya rushwa na ufisadi yaliyotamalaki kwenye nchi yetu katika miongo miwili iliyopita kwa sehemu kubwa chimbuko lake ni maamuzi haya ya CCM ya kufuta na kulizika kabisa Azimio la Arusha.”

Aliongeza,  “misingi na miiko muhimu iliyokuwa ndani ya Azimio hilo iliyowekwa kuhakikisha maadili ya uongozi yanakuwepo lakini CCM ilitupiliwa mbali kwa maslahi yao” alisema
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items