MCHEZAJI wa Simba Raia wa Ghana James Kotei, amekiri kuvutiwa na nahodha wake Jonas Mkude kwa jinsi anavyocheza mpira kwa kujituma pindi akiwa uwanjani.
Mkude ambaye alikuwa benchi wakati Simba ikicheza dhidi ya Prisons huku nafasi yake ikitendewa haki na Said Ndemla ambae alikuwa hapati namba katika kikosi cha kwanza mara kwa mara chini ya mwalimu Joseph Omog.
Kotei ameiambia shaffihdauda.co.tz kwamba, napenda namna Mkude anavyojituma katika nafasi yake ya kiungo ambayo anaonekana kuimudu vizuri.
“Mkude ni mchezaji mzuri, nimecheza nae mara kadhaa. Navutiwa sana kwa namna anavyojituma akiwa uwanjani,” alisema Kotei.
Aidha kiungo alisema ushindi wao dhidi ya Prisons umekuja kwa sababu timu yao ipo kwenye morali huku kila mchezaji akijawajibika ipasavyo ili kurudi katika nafasi yao ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
Video: Unaujua Uchungu wa Mke? Cheki hii ya Mau Fundi
