Naibu mwenyekiti wa Seneti Pakistan anyimwa viza ya Marekani

Maseneta wa Pakistan wafutilia mbali ziara yao Marekani baada ya serikali ya Trump kumnyima naibu mwenyekiti wa seneti kibali cha viza .

Maulana Abdul Ghafoor Haidri,ni naibu mwenyekiti wa seneti na pia katibu mkuu wa mojawapo ya vyama vikubwa zaidi cha kiislamu kitambulikacho kama Jamiat Ulema Islam (JUI).

Haidri alikuwa pamoja na wenzake wa seneti kuhudhuria mkutano uliodhamniniwa wa na UN katika mji wa New York hata hivyo ziara hiyo ilisitishwa baada ya kunyimwa kibali cha viza .

Tukio hilo limetokea wakati ambapo mahakama ya Marekani ilipiga marufuku sheria ya Trump ya kutoingiza raia kutoka mataifa 7 ambapo Pakistan haikuwa miongoni mwao.

Hata hivyo Marekani ilitoa viza kwa seneta mwengine wa Pakistan  kwa jina la  Salahuddin Tirmizi bila ya kutoa sababu maalum chanzo cha kumnyima kibali hicho Hadri.

Msemaji wa ubalozi wa Marekani Sharla Hussain Morgan aliambia shirika la habari la Anadolu kuwa hawana ruhusa ya kutoa maoni kuhusu kesi za binafsi za viza .



Video: Unaujua Uchungu wa Mke? Cheki hii ya Mau Fundi 



Mpya zaidi Nzee zaidi