Shehena kubwa ya bidhaa vikiwemo vinywaji vikali, maziwa ya watoto, vinywaji baridi na sigara vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 51 imeteketezwa jijini Mbeya baada ya kukamatwa zikiingizwa au kuuzwa nchini kinyume cha sheria.
Afisa mfawidhi wa forodha wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA, kitengo cha kuzuia magendo, Ernest Myenda, amesema bidhaa hizo zimeteketezwa baada ya kukamatwa na kubainika kuwa hazijasajiliwa nchini na mamlaka husika hivyo haziwezi kutozwa kodi kwa mujibu wa sheria.
Zoezi hilo la uteketezaji pia limezikumba sigara zenye thamani ya shilingi milioni sita ambazo zimetengenezwa nchini maalum kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi, lakini zikakamatwa zikiuzwa ndani ya nchi.
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA, imetoa rai kwa wafanyabiashara nchini kufuata sheria kwa kuuza bidhaa ambazo zimesajiliwa kwa lengo la kulinda afya za watanzania.