Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, Alhamis hii alipandishwa kizimbani kwenye mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jeshi lake bado lilimshikilia Wema na wenzake saba ambao walikamatwa na vielelezo na kuwa jalada lao lilipelekwa kwa wakili wa serikali alipitie ili aone ushahidi uliopo pamoja na kupata majibu kutoka kwa mkemia mkuu wa selikali kubaini kama kweli ni mtuamiji wa madawa ya kulevya.
Miongoni mwa mashtaka yanayomkali Wema Sepetu ni kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake.
