Baada ya kipigo cha mabao matatu kwa moja kutoka kwa vinara wa ligi Chelsea.Kelele nyingi zimeanza kuelekezwa katika kikosi cha Arsenal.Wapo wanaomshambulia kocha mkuu Wenger na kumtwisha zigo la lawama kutokana na kipigo hicho huku wengine wakiwabebesha lawama wachezaji wa timu hiyo kwamba hawajitumi.
Inaonekana hii imewachanganya wachezaji wa Arsenal sii tu ndani ya uwanja bali pia nje ya uwanja.Alex Ol-Chamberlain amejikuta matatizoni mtandaoni,Chamberlain ameingia katika matatizo hayo mara baada ya kipigo kutoka kwa Chelsea baada ya “kulike” tweet inayomtaka Wenger kuondoka.
Baada ya mechi kuisha kuna kurasa ya mashabiki wa Arsenal iitwayo Arsenal Fantv ilipost katika mtandao wa twitter.Post hiyo inasomeka “WENGER ANAPASWA KUONDOKA” moja kati ya watu ambao walike post hiyo kuonesha kukubaliana nayo alikuwa Ox Chamberlain.
Lakini baadae kupitia twitter tena Chamberlain alijitokeza kuomba radhi.Anadai hakujua anachofanya na hakuona kama alilike tweet hiyo japo baadhi ya wafuasi wake katika mtandao wa Twitter wanaonekana kutokukubaliana na kauli yake ya kusema hakuona na hakujua hata anachokifanya.
Kosa alilofanya Chamberlain ni kama limetonesha kidonda cha Wenger.Kwani sasa kelele nyingi zinamtaka Wenger aondoke Arsenal.Mbaya zaidi suala alilofanya Chamberlain linakuja wakati wakiwa wametoka kupigwa kipigo cha goli tatu kwa Chelsea.Haijafahamika saaa hadi sasa upi ni ukweli je ni Chamberlain anataka Wenger aondoke au kweli ilikuwa bahati mbaya.