Wagonjwa katika hospittali ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wodi ya wanawake wanajisaidia kwenye ndoo na vichaka kutokana na matundu ya vyoo kujaa kinyesi huku watunzaji wa wagonjwa wakilazimishwa kufua mashuka ya hospitali kwa mikono.
Hofu ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko imetanda kwa wagonjwa katika Hospitali ya wilaya ya Tunduru choo kinachotumika na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wanawake kuziba kwa kinyesi kwa zaidi ya wiki moja hali inayowafanya wagonjwa kujisaidia kwenye ndoo na wanaojiweza kwenye vichaka vya hospitali.
Wagonjwa hao wamesema kuwa hospitali haina maji wanalazimika kwenda kuchota nje ya geti huku wauguzi wakiwalazimisha ndugu wa wagonjwa kufua mashuka ya hospitali jambo linaloweza kuwasababishia kupata magonjwa ya kuambukiza.
Hayo yamebainika wakati viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tunduru walipotembelea hospitali hiyo kuwafariji wagonjwa ambapo walipaza sauti wakilalamikia kukithiri kwa uchafu unaotishia usalama wao.kutokana na changamoto hizo mkuu wa wilaya alitoa maagizo kwa mamlaka ya maji na uongozi wa hospitali huku akimtaka afisa ardhi kuripoti ofisini kwake.
Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Tunduru wamefanya maadhimisho ya miaka 40 ya kuyzaliwa kwa chama hicho kwa kuwatembelea wagonjwa na wafungwa na kuwapatia zawadi ya sabuni na vifaa tiba.