Jeshi la Polisi Dsm linawashilikia watuhumiwa 112 katika kipindi cha siku 3 katika Vita dhidi ya dawa za kulevya

Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm linawashilikia watuhumiwa 112 katika kipindi cha siku 3 katika Vita dhidi ya dawa za kulevya wakiwemo wasanii maarufu pamoja na kukamata kete 299 za dawa za kulevya na bangi puli 119 baada ya watuhumiwa waliokamatwa awali kushirikiana na jeshi hilo kuonyesha wauzaji wa dawa hizo.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dsm kamishna Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari amesema Msako huo ambao unaendelea bila kikomo umesaidia kubaini watu kadhaa vinara wanaojihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya lakini pia baadhi ya waliokamatwa kukiri kutumia dawa hizo na kuwataja baadhi ya watu wanaosambaza.

Aidha Kamishna Sirro amesema watuhumiwa 12 kati ya 112 watafikishwa mahakamani akiwemo wema Sepetu na Omar Michen ambao walibainika kukutwa na dawa za kulevya baada ya kupekuliwa,lakini pia watuhumiwa 10 watapelekwa mahakamani ili kupata kiapo cha hakimu ili wawe chini ya Uangalizi wa mahakama na jeshi la polisi katika kipindi cha miaka miwili.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda akizungumza katika mkutano huo ametoa siku 10 kwa wenyeviti wa serikali za mitaa na wazazi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kuwabainisha watumiaji au wauzaji wa dawa za kulevya kuanzia kesho.





VIDEO; USIPOCHEKA UTAKUWA MGONJWA

Mpya zaidi Nzee zaidi