Kocha maarufu nchini Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wanaomchamfua kuhusu kupiga 10% kwenye usajili wa wachezaji lengo lao ni kumchafua na kutaka aondoke sehemu ambapo alipo.
“Ni tuhuma ambazo watu wakitaka kukuchafua ili utoke sehemu, yani ni njia nyepesi ya kutaka kukutoa ni lazima wakutafutiekashfa ya kijinga ambayo haina maana.”
“Mimi naishi na wachezaji hata ukimuuliza mtu yeyote leo, nilikuwa na wachezaji wangu watu wanawaita wazee lakini mimi huwa nawajibu kuwa hawa wamecheza mpira kwa muda mrefu na ndio maana waliisaidia Mwadui kupanda.”
“Lakini sasa wakishatoka na kwenda sehemu nyingine wanasema Julio anaroho mbaya, lakini wanashindwa kujiuliza niliwachukuaje wakati mimi nina roho mbaya?”.
“Kwa mfano nikiwa Simba, mwenyekiti wa usajili ni Hans Poppe ambapo yeye ndio anazungumza kuelewana na mchezaji kuhusu dau la usajili na mshahara, sasa muulize Hans Poppe kawahi kunipa mimi hela mkononi nimpe mchezaji?”.
Kuna wakati Julio alikuwa anatuhumiwa kuomba wachezaji kiasi cha pesa zinazotokana na usajili wao ili wachezaji hao wasajiliwe kwenye klabu anayoifundisha kitu ambacho kocha huyo wa zamani wa Mwadui, Simba na timu za taifa amekikanusha.

VIDEO; Unaujua Uchungu wa Mke? Cheki hii ya Mau Fundi