Man United yamkosa Thomas Muller


IKIWA na miaka 16 kwenye kikosi cha Bayern Munich, Thomas Muller ni miongoni mwa washambuliaji hodari na ghari duniani na haishangazi kusikia Manchester United ikimtaka.

Jumatano usiku alikuwa mwiba mchungu kwa Arsenal alipofunga bao la tano dakika ya 88 ikiwa ni sekunde 120 baada ya kuingia dakik a ya 86 na kuiwezesha timu yake ya Bayern Munich kushinda mabao 5-1. Kabla ya mchezo huo kulikuwepo na habari za Man United inayofundishwa na Jose Mourinho kumuhitaji Muller kwenye kikosi chao tena wakaweka mezani dau la pauni milioni 85 sawa na Sh bilioni 232.

Mourinho baada ya kuwasajili Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na Paul Pogba kwa zaidi ya pauni milioni 145 (zaidi ya Sh bilioni 395.8) msimu huu, sasa anamtaka Muller ili kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji.

OFA YA MAN UNITED YAKATALIWA

Makamu Mwenyekiti wa Bayern Munich, Jan-Christian Dreesen klabu yake imepiga chini ofa ya Man United ya kutaka kumsajili Muller kwa ofa ya pauni milioni 85 ikisema bado inamuhitaji kikosini. Dreesen anayeshughulika zaidi na mambo ya fedha ya klabu hiyo, amethibitisha kushindwa kwa Mourinho katika mpango wake huo wa kumsajili Muller kwenda England kwa mara nyingine.

Alipotakiwa kuthibitisha kama alipokea ofa ya pauni milioni 85 kutoka Man United, Dreesen anasema:”Kuna kitu kama hicho, ikaja fax kutoka England. Kwetu sisi hatujawahi kuzungumza k u h u s u mauzo ya Thomas Muller, hatujazungumza lolote kumhusu yeye. ”

Kama mchezaji anatusaidia, tutakuwa wapuuzi tukimpa mkataba wa muda mfupi kutegemea na faida tutakayopata kutoka kwake.” Inaonekana Man United sasa imeanza harakati za kumtaka Muller kwa nguvu baada ya kuonekana kuna ugumu wa kumpata Antonio Griezmann wa Atletico Madrid kwani tayari kuna vikwazo kadhaa.



Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items