Mapinduzi ya Rais Magufuli yanazaa matunda-Makamba

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. January Makamba amesema kuwa mageuzi ambayo yamefanywa na Rais Magufuli toka ameingia madarakani yamezaa matunda

kwani na hiyo ni kutokana na jitihada za Rais Magufuli kuenzi misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
Wakijibu hoja zilizotokana na mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na maoni ya Wabunge Bungeni leo, Mawaziri wa sekta mbalimbali wamesisitiza kuwa kuna mabadiliko makubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Waziri Makamba amesema miezi 15 baadaye, na Bunge likiwa linajadili takwimu za robo ya kwanza tu ya Bajeti ya sasa, hata kama wapo watu ambao huenda wameumizwa na mageuzi yanayoendelea, kwa vyovyote vile, hakuna hoja wala ushahidi wa kulalamika kuwa nchi inarudi nyuma.



Mpya zaidi Nzee zaidi