Mkuu wa Mkoa Manyara amcharukia DC kisa migogoro ya Ardhi na Unyanyasaji

Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera ametoa wiki moja kwa uongozi wa wilaya ya hanang kutoa majibu juu ya unyanyasaji ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya wawekezaji kuwanyangíanya wananchi wenye uwezo mdogo mashamba yao.

Bendera anatoa kauli hii kwa uongozi wa wilaya ya hanang chini ya mkuu wa wilaya Sara msafiri katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano huu na kutoa fursa kwa wakaazi hawa wa hanang kueleza kero zao mbalimbali huku kilio cha maji pamoja na kero ya migogoro ya ardhi vikitawala.

Kwa upande mwingine Dkt Bendera akabainisha kuwepo jumla watu 25 wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya na hii inafuatia wananchi hawa kumshauri mkuu huyu wa mkoa kushughulikia tatizo la madawa.
Mpya zaidi Nzee zaidi