Lushoto. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema wameshindwa kuifikisha mahakamani kesi ya mbao 30 zilizokamatwa eneo la Dochi mjini Lushoto ambazo zinadaiwa kuwa ni mali ya halmashauri.
Mbao hizi zinadaiwa kutolewa kwenye karakana ya kutengeneza madawati na kupelekwa kwenye nyumba binafsi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Kazimbaya Makwega.
Kamanda Wakulyamba amesema wanaendelea kukusanya ushahidi na kwamba uliopo haujajitosheleza.
“Hatujalifikisha mahakamani suala hilo kwa kuwa ushahidi haujakamilika. Unajua gari ni la halmashauri na mbao hizo hatujajua mwenyewe ni nani, hivyo ni lazima tujiridhishe kabla ya kwenda mahakamani,” amesema.
Hata hivyo, Mkurugenzi Makwega alipoulizwa kuhusu sakata hilo, amesema mbao zilizokuwa zinapelekwa nyumbani kwake ni mali yake.
“Nimejenga nyumba eneo la Dochi tangu mwaka 2008 na hilo ni kutokana na mke wangu ambaye ni mwenyeji wa Lushoto na ni mtumishi wa Chuo cha Mahakama (IJA), hivyo watoto wangu wakija wasipate tabu, lakini nyumba hiyo bado nilikuwa sijamaliza dari,” amesema na kuongeza:
“Nilikuwa nikinunua mbao na kuzihifadhi kwenye karakana ya madawati na hilo ni kutokana na kule kwenye nyumba yangu usalama ni mdogo, hivyo mbao hizo nilizohifadhi kwenye karakana nikawa nachukua kidogokidogo. Sijui hizi shutuma kuwa nimechukua mbao za halmashauri zimetoka wapi.”