Sadick awaonya wajawazito wanaokuywa pombe

Hai. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick amewaonya wajawazito wanaokunywa pombe kuhakikisha kuwa wanakula chakula bora.

Sambamba na hilo amesema Serikali imeamua kuboresha vituo vya afya na hospitali kwa kuhakikisha zinakuwa na wataalamu wa kutosha ili kunusuru maisha ya wajawazito.

Akizungumza kwenye semina kuhusu uboreshaji wa huduma za afya, sadick amesema uboreshaji huo unalenga kuwanusuru akinamama na watoto.

“Nawakumbusha na kuwaonya wajawazito kuacha kunywa pombe za kienyeji na kusahau kula vyakula vyenye kujenga afya kwa kuwa baadhi ya wanywaji wapombe hizo pasipo kula wamekuwa wakipata utapiamlo na kusababisha kushindwa kujifungua salama,” alisema Sadick.

Awali, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Best Magoma amesema mapambano yanahitajika kutokomeza vifo vya wanawake wakati na kabla ya kujifungua.

Amesema utafiti uliofanywa Kilimanjaro mwaka 2014 unaonyesha kulikuwa na vifo 41 vilivyotokana na uzazi. Semina hiyo ya siku tatu imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya ya mama na mtoto.

Mpya zaidi Nzee zaidi