Mwanza. Tukio la kukamatwa zana haramu za uvuvi na baadaye kurejeshwa kwa wamiliki wake bila hatua kuchukuliwa limeibua utata jijini hapa.
Tukio hilo lililotokea Februari Mosi katika Mwalo wa Miembe Mitatu jijini Mwanza, limeibua tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa watendaji wa Idara ya Uvuvi, huku wakivutana na wa kitengo cha Kudhibiti na Kuzuia Uvuvi Haramu na Utunzaji wa Mazingira ya Ziwa Victoria (BMU).
Mjumbe wa BMU Kata ya Mkuyuni, Hamis Tibwa alisema kitendo cha Ofisa Uvuvi, Hussein Rugozi kuamuru zana hizo zirejeshwe kwa wavuvi kimewavunja moyo wa kupambana na uvuvi haramu.
“Hatuelewi kitu gani kilichotokea kwa sababu ni ofisa huyohuyo aliyetupigia simu twende kukamata zana hizo lakini muda mfupi baadaye akatuamuru kuzirejesha kwa wamiliki akidai ni maelekezo kutoka mamlaka ya juu,” alidai Tibwa aliyesema miongoni mwa zana hizo ni makokoro manane na mitumbwi minne.
Mvuvi aliyeshuhudia kukamatwa na kurejeshwa kwa zana hizo, Charles Fashion alisema kitendo hicho kinaweza kuhamasisha wavuvi wengine kuzitumia.
Rugozi akizungumzia tuhuma dhidi yake alisema aliamuru zirejeshwe ili kunusuru maisha yake na maofisa wenzake baada ya kuzingirwa na wavuvi waliojihami kwa silaha za jadi wakitishia kuwadhuru kutokana na zana zao kukamatwa.