TPRI yakamata shehena ya dawa za kuua wadudu zikiuzwa kiholela Mkoani Mtwara.

Wakaguzi kutoka taasisi ya udhibiti wa viuatilifu TPRI wamefanya ukaguzi kwenye wilaya za Tandahimba, Newala na Masasi na kukamata shehena za dawa zikiwa zinauzwa holela huku sehena ya  sumu hatari ya kuua wadudu kwenye maua ya  korosho aina ya Sulphur ikiwa imewekwa juani tena karibu na vyakula vya binadamu  kitendo kinacho tajwa kupunguza nguvu ya sumu hiyo na kuathiri  afya za binadamu.

ITV ilishuhudia shehena za viuatilifu vikiwa vimewekwa chini kwenye  maeneo yasiyo na sifa huku sumu aina ya Sulphur ikiwa imewekwa juani kwa muda mrefu hali inayotajwa kuathiri uwezo wa kuua wadudu  na kuwatia hasara wakulima wa Korosho.

Baadhi ya wauzaji walikutwa na makosa wakakiri kufanya makosa na kuahidi kufuata taratibu na mkaguzi wa TPRI kanda ya Dar-es-Salaam Solomoni Mungure akidai kuwa hali waliyo ikuta ni mbaya inabidi kuongeza nguvu ya operesheni.

Mpya zaidi Nzee zaidi