Serikali yathibitisha Watanzania 4 washikiliwa nchini Malawi kwa kufanya utafiti pasipo kibali

Serikali imesema watanzania wanane bado wanashikiliwa katika mahabusu za nchini Malawi kwa kuingia  nchini humo kinyume na taratibu na kufanya utafiti katika sehemu  yanapochimbwa madini ya Uranium  kinyume na taarifa zinazosambaa kuwa  walitumwa na serikali  kufanya shughuli za ujasusi nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano  wa kimataifa balozi Dr.Augustine Mahiga ameiambia ITV kuwa alikuwa nchini Malawi  kwa mambo mbalimbali ikiwemo kufuatilia kwa kina kuhusiana na watanzania hao na kwamba amekubaliana na rais wa nchi hiyo Mhe.Peter  Mutharika kuwa haki itendeke kwa watanzania hao.

Nao  baadhi ya wanasheria ambao ni watetezi wa haki za binadamu wamesema wanashangaa kukamatwa kwa watanzania hao kwani wao wanaamini kuwa waliingia kihalali nchini Malawi.




VIDEO: Unaujua Uchungu wa Mke? Cheki hii ya Mau Fundi 

Mpya zaidi Nzee zaidi