Spika Zziwa ashinda kesi

Arusha. Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imesema kanuni na utaratibu ulikiukwa kumuondoa madarakani Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Dk Margareth Zziwa Desemba 20, 2014.

Akisoma uamuzi kwa niaba ya majaji wenzake wanne, Jaji Kiongozi wa EACJ, Monica Mugenyi alisema Kanuni za Kudumu za Bunge na Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zilikiukwa hivyo hata spika aliyechaguliwa utaratibu haukufuatwa.

Hata hivyo, Jaji Mugenyi alisema  licha ya kujiridhisha katika ushahidi uliowasilishwa, Mahakama imejizuia kuingilia uhuru wa Bunge.

Alisema Ibara ya 53 ya Itifaki ya EAC  na kanuni za kudumu za Bunge hilo Ibara ya 9 vifungu vya 1,2,3 na 4, vinaeleza utaratibu wa kumuondoa Spika, lakini haukufuatwa kikamilifu, huku wakishindwa kupata ushauri wa mwanasheria wa EAC ambaye ni mshauri mkuu wa sheria.

Katika kesi hiyo namba 17 ya mwaka 2014 iliyofunguliwa na Dk Zziwa akipinga kuondolewa madarakani na wabunge wenzake, mlalamikiwa alikuwa Katibu Mkuu wa EAC. Aliiomba Mahakama hiyo itamke kurejeshwa kwenye nafasi yake na alipwe fidia.
Mpya zaidi Nzee zaidi