Baadhi ya wananchi wilayani Handeni mkoani Tanga wapo hatarini kupatwa na magonjwa ukiwemo ugonjwa wa Kimeta kutokana na kuwepo wimbi la wauzaji wa nyama kiholela zisizothibitishwa na wakaguzi wa bidhaa hiyo.
Hayo yamesemwa na mkaguzi wa nyama wilayani hapa Bi.Agness Nyange pamoja na hilo pia amezungumzia utoaji leseni wa biashara hiyo uzingatie ubora wa eneo husika lakini pia akagusia changamoto ya upatikanaji wa maji kwenye machinjio ya wilaya.
Kwa upande wao wafanya biashara wa kuuza nyama wamesema kuzaagaa kwa wafanya biashara hao holela wanaokwepa kodi inawaathiri kwani wateja wengi wa bidhaa hiyo hukimbilia kwa wauzaji hao kwa vile huuza bei ya chini kwa sababu hawalipi ushuru.

