Wakala Majengo Tanzania TBA,umesema umeshakamilisha ujenzi wa majengo yote ishirini ya mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam.
Jumla ya majengo 20 yenye ghorofa nne kila moja,yanayotarajiwa kuchukua wanafunzi 3,840 kati ya wananchuo 7,000 wanaolazimika kupanga vyumba vya kuishi mitaani,yanajengwa mashariki mwa chuo hicho.
Afisa mtendaji Mkuu wa Wakala Majengo Tanzania,Mhandisi ELIUS MWAKALINGA,katika mahojiano maalum na Channel Ten,iliyomtafuta kutaka kujua maendeleo ya mradi huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na jumuia ya Chuo kikuu cha Dar Es Salaam,amewahakikishia Watanzania kuwa mradi huo unaenda kama ilivyopangwa.
Mradi wa Ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam,ulianza kutekelezwa Julai Mosi mwaka jana na TBA,na kuwekwa jiwe la msingi na Rais dokta John Magufuli,oktoba 21 mwaka huo huo.
VIDEO: VUNJA MBAVU NA KINYAMBE ALIVYOJIFANYA MGANGA
