Baadhi ya watumiaji wa maji ya shirika la maji safi na maji taka Dar es salaam – Dawasco wamelalamikia usumbufu wanaopata kutoka Dawasco Kimara ikiwemo kuletewa ankara kubwa ukilinganisha na deni halisi ama matumizi yao jambo ambalo wamedai kuwa linawapotezea muda kila mara kwenda kufanya marekebisho katika ofisi hizo.
Wakizungumza na channel ten wateja hao wamesema adha nyingine wanayokabiliana nayo ni kitendo cha kutopewa risiti papo kwa papo mara baada ya kukabidhi risiti pindi wanapotoka benki kulipia huduma hiyo hususan kwa wale wanaoilipia kwa mkataba na kuambiwa waje kufuata risit ya Dawasco baada ya siku kadhaa.
Wamesema badala ya kufurahia huduma hiyo ambayo wameipata kwa shida bado wanakabiliwa na kibarua cha kufuatilia ankara zao halisi na wakati mwingine hutakiwa kwenda kuleta nakala za risit ambazo walipewa na Dawasco kwa ajili ya kurekebisha ankara hizo jambo ambalo linazua maswali mengi miongoni mwao kuwa huenda kitendo cha kutotoa risit papo kwa papo Kinachangia kupoteza kumbukumbu zao.
Channel Ten ilizungumza kwa njia ya simu na Meneja wa Dawasco Kimara ambaye amedai kuwa hajapata malalamiko hayo kutoka kwa wateja hao.