MUUGUZI Irene Machagge, jana alikwepa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kulipa faini ya Sh. 600,000, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mara kumtia hatiani kwa kosa la kughushi cheti cha elimu ya sekondari na kukitumia kuomba ajira.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Ofisa Uhusiano na Habari wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Makao Makuu, Mussa Misalaba, hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kalim Mushi, baada ya kusikiliza mashahidi wanne wa upande wa mashtaka na mshtakiwa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Hakimu Mushi aliamuru mshtakiwa afungwe jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh. 600,000 baada ya kumuona ana hatia.
Taarifa hiyo ya Takukuru inaeleza kuwa mshtakiwa huyo aliyekuwa akitetewa na Wakili Ostac Mligo, alilipa faini ya Sh. 600,000 na hivyo kukwepa kwenda jela kutumikia kifungo hicho.
Hakimu alisema aliridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri; bila kuacha shaka yoyote.
"Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Eric Kiwia, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake mwenyewe na watu wengine wenye tabia hiyo," taarifa hiyo inaeleza.
"Mshtakiwa aliiomba mahakama imwonee huruma kwa madai kwamba ni mjamzito na ana ugonjwa wa homoni ambao haumruhusu kukaa kwenye eneo lenye joto kali."
Taarifa hiyo inaeleza kuwa mshtakiwa alifikishwa mahakamani na Jamhuri kwa mara ya kwanza
Novemba 15, 2015 na kufunguliwa mashtaka mawili ya kughushi cheti cha elimu ya sekondari na kutumia cheti hicho kujipatia ajira ya uuguzi katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.
Taarifa ya Takukuru inaeleza kuwa awali ilidaiwa mahakamani na upande wa mashtaka kuwa kati ya
Mei na Septemba 2009, katika tarehe na maeneo yasiyofahamika, mshtakiwa alitenda kosa la kughushi cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Forodhani mwaka 1995.
Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa ilidaiwa Septemba 3, 2009, mshtakiwa aliwasilisha cheti kilichoghushiwa kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na hivyo kuajiriwa kuwa muuguzi katika hospitali hiyo.
Katika taarifa hiyo, inaelezwa kuwa wakati wa kutoa adhabu, Hakimu Mushi alisema amezingatia utetezi wa mshtakiwa, hivyo akamhukumu kulipa faini ya Sh. 500,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kwanza na faini Sh. 100,000 au kwenda jela miaka mitatu pia kwa kosa la pili.
"Hakimu Mushi alimhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini Sh. 600,000 kwa kuwa adhabu zinaenda pamoja," taarifa hiyo inafafanua.