F FFU Watumia Nguvu Kutuliza Ghasia Simiyu | Muungwana BLOG

FFU Watumia Nguvu Kutuliza Ghasia Simiyu

 WANAFUNZI takribani 600 wa Shule ya Sekondari ya Bariadi iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga Barabara Kuu ya Bariadi- Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Dues Toga.

Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri, lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi kuzuia ghasia (FFU) kuwazuia kwenda katika ofisi hizo.

 Askari wanne wa kutuliza Ghasia wakimdhibiti mwanafunzi

 Wakinesha bango kwa wanahabari
Kaimu mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akipokea bango kutoka kwa wanafunzi

Hata hivyo wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabaara hiyo waliamua kuandamana tena kuelekea ofisi za mkuu wa mkoa jambo lililoshindikana baada ya askari hao kuwazuia eneo la hospitali ya teule ya mkoa (Somanda)