F ALIYEDANGANYA FAMILIA YA MUMEWE KUWA NI MJAMZITO AKAMATWA KWA UWIZI WA MTOTO MCHANGA LUSHOTO. | Muungwana BLOG

ALIYEDANGANYA FAMILIA YA MUMEWE KUWA NI MJAMZITO AKAMATWA KWA UWIZI WA MTOTO MCHANGA LUSHOTO.

 


Na Rebeca Duwe , Lushoto.


Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Habiba Seleman Fundi kwa tuhuma za wizi wa mtoto mchanga katika hospitali ya wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.


Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga  Almachius Mchunguzi alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 21juni mwaka huu Majira ya saa 1 usiku katika kitongoji cha Garekaya Wiliyani Lushoto akiwa na mtoto  huyo.


Kamanda Mchunguzi alisema alisema kuwa manamo juni 19 mwaka huu saa 11jioni mama mzazi wa mtoto huyo Mwanaidi Juma Nyaki mkazi wa Kijiji cha Kwemakame aliripoti kupotea kwa mwanae wa siku moja .


Aidha  aliongeza kusema kuwa mtuhumiwa huyo alitumia mbinu ya kujenga urafiki wa  karibu na mama mzazi wa mtoto huyo pamoja ndugu waliokuwa wakimhudumia hospitalini hapo.


Alisema baada ya kupata imani yao alichukua fursa hiyo na kumweka mtoto ndani ya beseni lenye nguo  kisha kutoweka na mtoto bila kufahamika kwa wakati huo.


Sambamba na hayo alisema uchunguzi wa kina umebaini kuwa mtuhumiwa alikuwa akidai kwa muda mrefu kuwa ni mjamzito na kuwahakikishia  ndugu,jama wa mume wake kuwa alikuwa akisubiri kujifungua.

 

Hata hivyo baadaya muda ameuweka kufika aliamua kufanya mpango huo wa kuiba mtoto ili kuwathibitishia madai yake kwa familia  ya mumewe na watu waliokuwa wakimzunguka kuwa alikuwa mjamzito na amejifungua.


mwisho

Chapisha Maoni

0 Maoni