January Makamba atoa agizo zito Korogwe

Korogwe/Same. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amewaagiza wakazi wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, kuvilinda vyanzo vya maji vilivyopo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Makamba ambaye yupo ziarani katika mikoa ya kaskazini, amesema ili kuhifadhi mazingira, ni vyema kukawepo na uhifadhi wa vyanzo vya maji na kuitaka kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kukutana na kujadili suala hilo kwa kina.

Baada ya kutoka wilayani humo, waziri huyo amekwenza katika Wilaya ya Same iliyopo mkoani Kilimanjari na kupata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwamo Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na Shule ya Msingi Majevu ambayo paa lake liliezuliwa na mvua.

Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Senyamule amemwambia Makamba kuwa uingizaji wa mifugo na katika makazi ya watu na chomaji wa  misitu ni miongoni mwa mambo yanayochangia uharibifu wa mazingira katika wilaya hiyo.

Rosemary amesema kutokana na hali hiyo wameanza kuwadhibiti watu hao, lakini jitihada zaidi zinahitajika kwa sababu uharibifu wanaoufanya ni mkubwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items