Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Maurcio Pochettino amesema kuwa kamwe hatoifundisha klabu ya Barcelona kutokana na mapenzi yake na klabu yake ya zamani ya Espanyol, ambao ni wapinzani wakubwa na Barca.
Pochettino ambaye ni raia wa Argentina amesema pia hatoifundisha Arsenal kwa sababu ni wapinzani wakubwa wa Spurs.
Pochettino, 45, pia alichezea Espanyol mechi 216.
Katika kikao na wanahabari Alhamisi Pochettino alisema: “Ni kama siku moja, iwapo (mwenyekiti wa Spurs) Daniel Levy atanifuta kazi, haiwezekani kwangu kuwa mkufunzi wa Arsenal.”
Taarifa zinasema Spurs walifahamu kuhusu mkutano wa Pochettino na rais huyo wa Barca.
Mkufunzi msaidizi wa Barca Juan Carlos Unzue anapigiwa upatu kumrithi Enrique ambaye anaondoka mwisho wa msimu.
Mkufunzi wa Athletic Bilbao Ernesto Valverde pia anaaminika kuwa miongoni mwa wale ambao wanaweza kupewa kazi hiyo.