F Mbunge CHADEMA afichua siri kilimo cha Bangi | Muungwana BLOG

Mbunge CHADEMA afichua siri kilimo cha Bangi


MBUNGE wa   Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema), ametoboa siri ya kilimo cha bangi wilayani humo hususan eneo la Nkongore Kata ya Kitare.

Amesema  zao hilo lilikuwa likilimwa na raia  kutoka Kenya ambao walikuwa wakikodi ardhi Tanzania.

Pia aliitaka Serikali kufanya   utafiti kuhusiana bangi na tumbaku   iwapo kuna athari kubwa na kupendekeza kuangalia uwezekano wa kulifanya zao hilo kuwa la biashara.

 Alisema baada ya jeshi la polisi kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo,  Glorius Luoga, kuteketeza zao hilo. alikwenda kutembelea wakazi hao.

Matiko alisema kwa mujibu wa maelezo ya wakazi wa eneo hilo la Nkongore, raia  kutoka Kenya ndiyo walikuwa wakikodi ardhi  hiyo kwa ajili ya kilimo  cha bangi  kwa vile   zao hilo lina soko kubwa Kenya na  mataifa mengine jirani.

“Raia wa Kenya wanakuja Tarime kwa sababu ya ardhi ipo  na  ina rutuba nzuri lakini jambo ambalo nimekuwa nikilipigia kelele hata bungeni ni kwamba  hilo zao linapaswa kuruhusiwa kulimwa kwa sababu lina soko kubwa nje ya nchi.

“Nilisema katika Bunge la 10 nikaiomba Serikali ifanye utafiti au ilete ushahidi kati ya bangi na tumbaku kipi kina madhara makubwa.

“Leo ukiitaka Serikali ilete mtu mmoja tu ambaye alitumia bangi na kuwa teja hawezi kupatikana, naishauri Serikali iruhusu bangi ilimwe kwa lengo la kuuzwa nje ya nchi,”alisema.

Matiko alisema ikiwa zao hilo litaruhusiwa na kuweka mipango namna ya ulimaji na usafirishaji litaweza kuliingizia kipato taifa kuliko baadhi ya mazao yanayopewa kipaumbele.

 Alisema   siyo kwamba anapingana na Serikali juu ya mapambano ya dawa za kulevya nchini, bali anataka  uwepo mpango  madhubuti wa kuangalia zao la bangi ambalo madhara yake ni kidogo kuliko ilivyo kwa tumbaku.

Alisema Tarime haina vyanzo vingi vya mapato na ndiyo maana kuna baadhi ya maeneo maendeleo yamekwema.

Mbunge huyo aliiomba Serikali kufungua mnada wa ng’ombe wa Magena   mpakani na Kenya.

Alisema mnada huo ulifungwa kisiasa kutokana na kile kilichodai unatumika   kurahisisha vitendo vya wizi wa ng’ombe kutoka Tanzania kwenda Kenya.

Hata hivyo, alisema baada ya kupiga kelele hivi karibuni bungeni,   viongozi wa Serikali walifika eneo hilo mwishoni mwa mwaka jana na kuahidi kuufungua.

Alisema soko la kimataifa la Lemagwe lilipo wilayani humo nalo limeshindwa kufanya kazi na kusababisha ajira kupotea   huku miundombinu yake ikianza kuharibika.




Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote, Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... 

Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako... USIWE NA WASIWASI HUDUMA HII NI SALAMA KABISA..