Miili ya wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa inaaminika kupatikana katika eneo walipokuwa wametekwa nchini DRC.
Wafanyakazi hao wawili wa UN Michael Sharp na Zaida Catalan walitekwa nyara wiki mbili zilizopita.
Mmoja wao ni Mmarekani na mwingine kutoka Sweden,wakiwa wote ni wazungu.
Wafanyakazi hao wa Umoja wa Mataifa,kwa mujibu wa habari walikuwa katika eneo la Kasai ili kufanya uchunguzi kuhusu ripoti za dhuluma nchini humo.
Eneo la Kasai limekuwa na ghasia na fujo sana siku chache zilizopita kwani ni eneo hilohilo ambapo maaskari 40 waliuawa kwa kukatwa vichwa.
Ghasia nchini DRC zinaaminika kuletwa na mzozo kati ya Serikali na kundi la upinzani.
Kumekuwa na tafrani kati ya serikali na wafuasi wa kiongozi wa kitamaduni aliyeuawa Kamuina Nsapu.
Kamuina Nsapu alikuwa ni kiongozi aliyempinga Rais Joseph Kabila.