Mishipa ya miguu yapandikizwa kwenye moyo

Dar es Salaam. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Saifee ya India wamewafanyia watu wanane upasuaji wa kuvuna mishipa ya miguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba.

Akizungumza leo,Daktari Bingwa wa Moyo wa taasisi hiyo, Bashir Nyangasa amesema watu wanane wamefanyiwa upasuaji na wanaendelea vizuri.

Amesema madaktari sita kutoka India na wenzao kutoka katika taasisi hiyo wamebadilishana uzoefu katika zoezi hilo lililoanza Jumatatu hadi jana.

Kiongozi wa madaktari hao kutoka India,Dk Aliasgar Behranwala amesem taasisi JKCI ina mazingira mazuri kwa madaktari kufanya kazi   za upasuaji wa moyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items