https://monetag.com/?ref_id=TTIb Sarafu Kubwa ya Dhahabu ya Malkia Elizabeth Yaibiwa Ujerumani | Muungwana BLOG

Sarafu Kubwa ya Dhahabu ya Malkia Elizabeth Yaibiwa Ujerumani

UJERUMANI: Sarafu kubwa na nzito iliyotengenezwa kwa madini ya dhahabu, ambayo ina picha ya Malkia Elizabeth wa Uingereza, ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 4 (Pound Euro milioni 3.2) ambazo ni sawa na TZS bilioni 8.9, imeibiwa kutoka kwenye makumbusho ya Ujerumani.

Sarafu hiyo kutoka Canada ambayo mtu mmoja hawezi kuibeba, inathaminishwa kwa dola milioni 1, lakini kwa sababu imetengenezwa kwa kilo 100 za dhahabu, thamani yake ni ya juu zaidi kwa kutumia bei ya sasa ya dhahabu.

Iliibiwa usiku kutoka makavazi ya Bode mjini Berlin ambapo mpaka sasa bado haijabainika ni kwa namna gani wezi walifanikiwa kuingia bila kugunduliwa na mtambo wa kuzuia wezi, na kisha wakafanikiwa kutoroka na sarafu hiyo ambayo nusu kipenyo chake ni cha nusu mita.

Wizi huo unaaminika kutekelezwa majira ya saa 9:30 alfajiri Jumatatu, ambapo polisi wa eneo hilo wanasema huenda polisi waliingia kupitia dirisha.

Ngazi ilipatikana imetupwa kwenye reli iliyo karibu, msemaji wa polisi Winfrid Wenzel aliambia Reuters. “Sarafu hiyo ilikuwa imehifadhiwa ndani ya sehemu isiyoweza kupenya risasi ndani ya makumbusho,” alisema mmoja wa polisi hao. Sarafu hiyo ilifuliwa mwaka 2007 na Royal Canadian Mint.