Shilingi 605.34 milioni za TACAIDS zatumikwa kwa mapambano dhidi ya UKIMWI halmshauri ya wilaya ya Lindi

Na.Ahmad Mmow.
KATIKA kukabiliana na gonjwa hatari la UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Lindi.Halmashauri hiyo imetumia shilingi 605,345,864/- zilizotolewa na tume ya taifa ya k udhibiti UKIMWI(TACAIDS) kwa halmashauri hiyo kuanzia mwaka  2008 hadi  2016.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa mapambano dhidi ya UKIMWI wa halmashauri hiyo,Yolenda Mkumbuli alipokuwa anaeleza changamoto na mafanikio yaliyopatikana dhidi ya mapambano hayo.

Alisema kiasi hicho cha fedha ambacho kilikuwa kinapokewa kila mwaka kuanzia mwaka 2008 hadi mwakajana kilic hangia kupungua kwa maambukizo ya Virusi Vya UKIMWI(VVU) baada ya jamii kupokea elimu na kuhamasika kupima afya kwa hiari.

Alisema jamii wilayani humo imepatiwa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya ya kujikinga na namaambukizi mapya ya VVU katika makundi yote ya kijamii.

Ikiwemo  ya vijana na walemavu."Jamii imehamasika kupima afya zake,nawale wenye maambukizi ya VVU wamejiunga pamoja katika vikundi vya ujasiriamali.Mpaka sasa kuna vikundi 40 vya watu waishio na Virusi Vya UKIMWI ambavyo vina wanachama 522,"alisema Yolenda.

Alisema juhudi kubwa zilizofanyika kupita fedha hizo na zanazotokana na vyanzo vya ndani vya mapato vya halmashauri hiyo zimesababisha kupungua kwa maambukizi ya VVU mwaka hadi mwaka.

Ambapo hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana kiwango cha maambukizo kilishuka hadi kufikia 3.6% kutoka  7.2% cha mwaka 2008.

Aliyataja baadhi ya matumizi ya fedha hizo na mafanikio kuwa ni wanachama wa vikindi vya wanaoishi na VVU kupata elimu ya ujasriamali kwa kutumia ruzuku iliyowawezesha kujikwamua kiuchumi na kusababisha kuboresha afya zao kiasi cha kushiriki kazi za uzalishaji mali.

Ikiwamo kilimo,ufugaji, biashara na wengine kijiunga katika VICOBA."Watoto 200 waliokuwa wakiishi katika mazingira hatarishi wamepata msaada kwa kulipiwa karo za shule na kununuliwa mahitaji muhimu kupitia fedha hizo,nakuwawezesha wapate elimu kama watoto wengine,"alibainisha Yolenda.

Aliongeza kusema fedha hizo pia zimesababisha watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo kupata elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi, kupitia mpango wa utoaji elimu mahali pakazi.Ambapo wenye waliothibitika kuwa na maambukizi na walioamua kuweka wazi kwa mwajiri wao walipata huduma zinazositahili kwa mujibu wa waraka namba 2 wa mwaka 2006.

Huku kila mmoja akipatiwa shilingi 50,000/- kila mwezi.Yolenda ambae alisema  halmashauri hiyo imetenga shilingi 15,000,000/- kupitia mapato ya ndani ili kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI.

Alisema miongoni mwa changamoto ni kukoma kwa mradi huo tangu mwaka kumesababisha kutofikiwa kwa malengo yaliyotarajiwa kutokana halmashauri kubeba mzigo mkubwa wa kukamilisha shuguli mbalimbali ambazo zilianza kwa kutumia fedha hizo.

Halmashauri ya Lindi yenye ukubwa wa kilometa za mraba 6623 yenye wakazi 194143 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 imeweza kufikisha elimu kwa jamii katika kata zote 31.Ambapo kata 28 kati ya hizo zimefanikiwa kuunda vikundi vya watu wanaoishi na VVV

Mpya zaidi Nzee zaidi