Saa kadhaa baada ya Rais John Pombe Magufuli kumuapisha Waziri mpya wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba, kumekuwa na taarifa inayoenea mitandaoni ikieleza kuwa imetoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa ameikanusha taarifa inayosambaa ikionyesha kuwa serikali inatishia kuifuta mitandao ya kijamii.
Taarifa hiyo iliyoonyesha imeandaliwa na Ikulu, ilieleza kuwa serikali haitasita kuifuta mitandao ya kijamii iwapo itabaini kuwa yote yanayoendelea hayana tija.
“Serikali inafuatilia kwa karibu yote yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii, na endapo itabaini haina tija,
Msigwa baadaye aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akiwataka watanzania waipuuze taarifa hiyo kwa kuwa ni feki.


